Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ (ONMM 2024)

Zaburi 14

Read Scripture freely. Divine Threads study for this chapter is coming later.

1Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wamepotoka, matendo yao ni maovu kabisa; hakuna hata mmoja atendaye mema.
2Mwenyezi Mungu anawachungulia wanadamu kutoka mbinguni aone kama kuna mwenye hekima, yeyote anayemtafuta Mungu.
3Wote wamepotoka, wote wameoza pamoja; hakuna atendaye mema, naam, hakuna hata mmoja!
4Je, watendao maovu kamwe hawatajifunza: wale ambao huwala watu wangu kama watu walavyo mkate, hao ambao hawamwiti Mwenyezi Mungu?
5Wako hapo, wameingiwa na hofu kuu, maana Mungu yupo pamoja na wenye haki.
6Ninyi watenda maovu mnakwamisha mipango ya maskini, bali Mwenyezi Mungu ndiye kimbilio lao.
7Laiti wokovu wa Israeli ungekuja kutoka Sayuni! Mwenyezi Mungu anaporejesha wafungwa wa watu wake, Yakobo na ashangilie, Israeli na afurahi!