Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ (ONMM 2024)

Zaburi 13

Read Scripture freely. Divine Threads study for this chapter is coming later.

1Hadi lini, Ee Mwenyezi Mungu? Je, utanisahau milele? Utanificha uso wako hadi lini?
2Nitapambana na mawazo yangu hadi lini, na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu? Adui zangu watanishinda hadi lini?
3Nitazame, unijibu, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu. Yatie nuru macho yangu, ama sivyo nitalala usingizi wa mauti.
4Adui yangu atasema, “Nimemshinda,” nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka.
5Lakini ninategemea upendo wako usiokoma; moyo wangu unashangilia katika wokovu wako.
6Nitamwimbia Mwenyezi Mungu, kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.