Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ (ONMM 2024)

Zaburi 15

Read Scripture freely. Divine Threads study for this chapter is coming later.

1Mwenyezi Mungu, ni nani awezaye kukaa katika Hekalu lako? Nani awezaye kuishi katika mlima wako mtakatifu?
2Ni yule aendaye pasipo mawaa, atendaye yaliyo haki, asemaye kweli toka moyoni mwake,
3na hana masingizio ulimini mwake, asiyemtenda jirani yake vibaya, na asiyemsingizia mwenzake,
4ambaye humdharau mtu mbaya, lakini huwaheshimu wale wamwogopao Mwenyezi Mungu, yule atunzaye kiapo chake hata kama anaumia.
5Yeye akopeshaye fedha yake bila riba, na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia. Mtu afanyaye haya kamwe hatatikisika.