Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ (ONMM 2024)

Zaburi 12

Read Scripture freely. Divine Threads study for this chapter is coming later.

1Mwenyezi Mungu tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka; waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu.
2Kila mmoja humwambia jirani yake uongo; midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu.
3Mwenyezi Mungu na akatilie mbali midomo yote ya hila na kila ulimi uliojaa majivuno,
4ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda; midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?”
5“Kwa sababu wanyonge wanaonewa, na wahitaji wanalia kwa uchungu, nitainuka sasa,” asema Mwenyezi Mungu. “Nitawalinda kutokana na wale wenye nia mbaya juu yao.”
6Maneno ya Mwenyezi Mungu ni safi, kama fedha iliyosafishwa katika tanuru, iliyosafishwa mara saba.
7Ee Mwenyezi Mungu, utatuweka salama na kutulinda na kizazi hiki milele.
8Watu waovu huenda wakiringa kila mahali wakati yule aliye mbaya sana ndiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu.