Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ (ONMM 2024)

Zaburi 134

Read Scripture freely. Divine Threads study for this chapter is coming later.

1Msifuni Mwenyezi Mungu, ninyi nyote watumishi wa Mwenyezi Mungu, ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu.
2Inueni mikono yenu katika patakatifu na kumsifu Mwenyezi Mungu.
3Naye Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na dunia, awabariki kutoka Sayuni.