1Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!
2Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, yakitiririka kwenye ndevu, yakitiririka kwenye ndevu za Haruni, hadi kwenye upindo wa mavazi yake.
3Ni kama umande wa Hermoni ukianguka juu ya Mlima Sayuni. Kwa maana huko ndiko Mwenyezi Mungu alikoamuru baraka yake, naam, uzima hata milele.