Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ (ONMM 2024)

Zaburi 54

Read Scripture freely. Divine Threads study for this chapter is coming later.

1Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, unifanyie hukumu kwa uwezo wako.
2Ee Mungu, sikia maombi yangu, usikilize maneno ya kinywa changu.
3Wageni wananishambulia, watu wakatili wanayatafuta maisha yangu, watu wasiomjali Mungu.
4Hakika Mungu ni msaada wangu, Bwana ndiye anayenitegemeza.
5Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia, kwa uaminifu wako uwaangamize.
6Nitakutolea dhabihu za hiari; Ee Mwenyezi Mungu, nitalisifu jina lako kwa kuwa ni vyema.
7Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote, na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi.