Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ (ONMM 2024)

Zaburi 4

Read Scripture freely. Divine Threads study for this chapter is coming later.

1Nijibu nikuitapo, Ee Mungu wangu mwenye haki! Nipumzishe katika shida zangu; nirehemu, usikie ombi langu.
2Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangu kuwa aibu hadi lini? Mtapenda udanganyifu na kufuata miungu ya uongo hadi lini?
3Fahamuni hakika kwamba Mwenyezi Mungu amewatenga wale wamchao kwa ajili yake; Mwenyezi Mungu atanisikia nimwitapo.
4Katika hasira yako, usitende dhambi. Tulieni kimya mkiwa vitandani mwenu, mkiichunguza mioyo yenu.
5Toeni dhabihu zilizo haki; mtegemeeni Mwenyezi Mungu.
6Wengi wanauliza, “Ni nani awezaye kutuonesha jema lolote?” Ee Mwenyezi Mungu, tuangazie nuru ya uso wako.
7Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi.
8Nitajilaza chini na kulala kwa amani, kwa kuwa wewe peke yako, Ee Mwenyezi Mungu, waniwezesha kukaa kwa salama.