Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ (ONMM 2024)

Zaburi 130

Read Scripture freely. Divine Threads study for this chapter is coming later.

1Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Mwenyezi Mungu.
2Ee Bwana, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie.
3Kama wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ungeweka kumbukumbu ya dhambi, Ee Bwana, ni nani angeweza kusimama?
4Lakini kwako kuna msamaha, kwa hiyo wewe unaogopwa.
5Namngojea Mwenyezi Mungu, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu.
6Nafsi yangu inamngojea Bwana kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi, naam, kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi.
7Ee Israeli, mtumaini Mwenyezi Mungu, maana kwa Mwenyezi Mungu kuna upendo usiokoma, na kwake kuna ukombozi kamili.
8Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli kutoka dhambi zao zote.