1Mwenyezi Mungu asipoijenga nyumba, wajengao hufanya kazi bure. Mwenyezi Mungu asipoulinda mji, walinzi wakesha bure.
2Mnajisumbua bure kuamka mapema na kuchelewa kulala, mkitaabikia chakula: kwa maana yeye huwapa usingizi wapendwa wake.
3Watoto ni urithi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu, uzao ni zawadi kutoka kwake.
4Kama mishale mikononi mwa shujaa ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.
5Heri mtu ambaye podo lake limejazwa nao. Hawataaibishwa wanaposhindana na adui zao langoni.