1Nilishangilia pamoja na wale walioniambia, “Twende nyumbani mwa Mwenyezi Mungu.”
2Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama malangoni mwako.
3Yerusalemu imejengwa vyema kama mji ulioshikamana pamoja.
4Huko ndiko makabila hukwea, makabila ya Mwenyezi Mungu, kulisifu jina la Mwenyezi Mungu kulingana na maagizo waliopewa Israeli.
5Huko viti vya hukumu hukaa, viti vya ufalme vya nyumba ya Daudi.
6Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu: “Wote wanaokupenda na wawe salama.
7Amani na iwe ndani ya kuta zako, na usalama ndani ya ngome zako.”
8Kwa ajili ya ndugu na rafiki zangu, nitasema, “Amani iwe ndani yako.”
9Kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, nitatafuta mafanikio yako.