Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ (ONMM 2024)

Zaburi 110

Read Scripture freely. Divine Threads study for this chapter is coming later.

1Mwenyezi Mungu amwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowafanya adui zako kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”
2Mwenyezi Mungu ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni; utatawala katikati ya adui zako.
3Askari wako watajitolea kwa hiari katika siku yako ya vita. Ukiwa umevikwa fahari takatifu, kutoka tumbo la mapambazuko utapokea umande wa ujana wako .
4Mwenyezi Mungu ameapa, naye hatabadilisha mawazo yake: “Wewe ni kuhani milele, kwa mfano wa Melkizedeki.”
5Bwana yuko mkono wako wa kuume, atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.
6Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga na kuwaponda watawala wa dunia nzima.
7Atakunywa maji katika kijito kando ya njia ; kwa hiyo atainua kichwa chake juu.