Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ (ONMM 2024)

Zaburi 1

Read Scripture freely. Divine Threads study for this chapter is coming later.

1Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hasimami katika njia ya wenye dhambi, au kuketi katika baraza la wenye mizaha.
2Bali huifurahia Torati ya Mwenyezi Mungu, naye huitafakari hiyo Torati usiku na mchana.
3Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda kwa majira yake na majani yake hayanyauki. Lolote afanyalo hufanikiwa.
4Sivyo walivyo waovu! Wao ni kama makapi yanayopeperushwa na upepo.
5Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu, wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.
6Kwa maana Mwenyezi Mungu huziangalia njia za mwenye haki, bali njia za waovu zitaangamia.